Afisa mkuu Ezra Chiloba atakiwa ajibu maswali


Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amemwandikia barua afisa mkuu Ezra Chiloba akimtaka kueleza ni kwa nini changamoto na makosa yalitokea katika uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita. Barua hiyo inajiri wakati ambapo makamishna wa tume hiyo wamekuwa wakizozana kutokana na hatua ambazo mwenyekiti Chebukati amechukua katika maandalizi ya uchaguzi wa urais ujao huku kinyang’anyiro hicho kikikisiwa kugharimu taifa hadi shilingi bilioni 13. Hata hivyo makamishna watano wa tume hiyo wamekanusha kuwa Chebukati alimtumia Chiloba barua hiyo.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Different journeys, same destiny: The story of top two candidates | KCSE 2020 |

Avatar
Story By Sam Gituku
More by this author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *