Afisi ya naibu rais Ruto yatangaza zabuni ya kukodisha ndege


Afisi ya naibu rais Ruto yatangaza zabuni ya kukodisha ndege
File photo of Deputy President William Ruto. PHOTO| DPPS

Afisi ya Naibu wa Rais William Ruto imetangaza kuwa inapokea maombi ya wanaonuia kukodisha helikopta na ndege wastani kwa afisi yake.

Katika tangazo la zabuni hiyo, afisi ya naibu wa rais imewarai watoaji huduma hiyo kuchukua stakabadhi za maombi kutoka jumba la harambee orofa ya kwanza chumba cha 1b12/13 pamoja na kulipa shilingi elfu moja kwa katibu mkuu wa usimamizi afisi ya naibu wa rais.

Wanaotaka kutuma maombi wanastahili kufanya hivyo kabla tarehe 23 mwezi huu saa nne asubuhi.

Tangazo hili linajiri wakati ambapo serikali imetangaza kupunguza gharama ya matumizi ya fedha huku ushuru kwa bidhaa za mafuta ikiongezwa katika sheria ya fedha iliyotiwa saini na rais Uhuru Kenyatta wiki mbili zilizopita.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: | PAIN IN SERVICE | Frontline workers narrate the ordeal of fighting Covid-19

Avatar
Story By Mashirima Kapombe
More by this author