Asilimia 63 ya mahindi katika maghala ya NCPB hayafai kutumika na binadamu

Asilimia 63 ya mahindi katika maghala ya NCPB hayafai kutumika na binadamu

Takriban asilimia 63 ya mahindi katika maghala ya NCPB  hayafai kutumika na binadamu. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya bodi ya kutathmini ubora wa bidhaa nchini, KEBS.

Hata hivyo, akiongea mbele ya  kamati maalum ya Bunge la Senate kuhusu hali ya kilimo cha mahindi nchini, Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri amesema hawawezi kuharibu mahindi hayo kwani wataalam wametofatiana kuhusu ubora wa mahindi hayo.

Kiunjuri hata hivyo amejiondolea lawama kutokana na masaibu yanayokumba sekta hiyo na badala yake kumlaumu aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Felix Koskei.

Anasema magunia milioni 10.4 yaliagizwa kutoka mataifa ya nje kinyume na magunia milioni 6 yaliyokuwa yamekusudiwa

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories