“Askofu” Deya ashtakiwa hatia ya kuiba watoto


Baada ya kukwepa mashtaka kwa zaidi ya mwongo mmoja, akiwa nchini Uingereza Askofu Gilbert Deya hatimaye amerejeshwa humu nchini kukabiliana na mashtaka ya jinai.
Askafu huyo anakabiliwa na mashtaka matano ya wizi wa watoto yanayoaminika kutekelezwa humu nchini kati ya mwaka wa 1999 na 2004. Deya alirejeshwa humu nchini mapema hii leo, na kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye makao makuu ya CID kabla ya kufikishwa mahakamani muda mfupi baadaye.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: The Fresh Look 9PM Bulletins... #ThisIsTheStory

Story By Patrick Igunza
More by this author