

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kuwakumbuka manusura na waathiriwa wa ajali za barabarani hapo kesho, eneo la Salgaa katika kaunti ya Nakuru linazidi kuwakosesha usingizi madereva, abiria na wenyeji kutokana na ajali za mara kwa mara katika eneo hilo. Japo takwimu zinaonesha kuwa idadi ya ajali za barabarani imepungua ikilinganishwa na mwaka jana, eneo la Salgaa limeifanya kaunti ya Nakuru kuwa ya pili katika wingi wa ajali nchini.
Video Of The Day: Treasury allocates Ksh 4.5 B for procurement of vaccines