Bodi ya NGO yatishia kutwaa leseni ya KHRC
Published on: January 07, 2017 07:49 (EAT)
Bodi ya baraza la mashirika yasiyo ya kiserikali imetoa ilani ya kufutiliwa mbali kwa leseni ya tume ya kutetea haki za kibinadamu-KHRC. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na bodi hiyo, KHRC inadaiwa kukiuka kanuni mbalimbali zilizowekwa, kuwa na akaunti haramu za benki na kutolipa ushuru wa shilingi milioni mia moja. Hata hivyo KHRC imetaja madai hayo kuwa ya uongo na kutishia kumshtaki mkurugenzi wa bodi hiyo Fazul Mohammed.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment