Chama cha Jubilee chazindua timu yake ya kampaini Pwani

Chama cha jubilee kimezindua kikosi maalum kitakachofanikisha juhudi za kusaka kura na kuipigia debe azma ya Rais Uhuru Kenyatta ya kupata muhula mpya mwaka ujao.

Naibu wa rais william ruto aliyeongoza juhudi hizo alisema kuna mwamko mpya kisiasa katika eneo la Pwani, ambalo limekuwa ngome ya muungano wa Cord.

Kando na kugusia miradi ya maendeleo ambayo serikali imeanzisha katika eneo la Pwani, viongozi wa jubilee waliikaripia Cord na kinara Wake Raila Odinga kwa kile walichodai ni siasa za porojo na kupinga maendeleo. Francis Gachuri una taarifa kamili kutoka Mombasa.

Tags:

JUBILEE

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories