Chebukati ataka Raila na Uhuru wazungumze
Published on: October 18, 2017 08:37 (EAT)
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati sasa anasema hawezi kuwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi wa wiki ijayo utakuwa huru na wa haki iwapo hali iliyopo haitabadilika. Chebukati amelalamikia mgawanyiko baina ya makamishna kwa misingi ya kisiasa na kazi ya IEBC kuhujumiwa na serikai na upinzani. Hata hivyo, amesema kuwa hatojiuzulu na atajaribu awezavyo kufanya kazi yake akiongozwa na katiba na sheria. Kauli hiyo ya Chebukati inajiri baada ya kamishna Roselyn Akombe kujiuzulu.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment