Chebukati: Mkurugenzi wa ICT, James Muhati atimuliwe


Uamuzi kamili wa mahakama ya upeo ukisubiriwa, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati sasa anapendekeza kusimamishwa kazi kwa maafisa watatu wanaohusika na habari na teknolojia. Chebukati anasema kuwa uchunguzi wa ndani kwa ndani wa IEBC unaonyesha kuwa mkurugenzi wa habari na teknolojia James Muhati, mshirikishi Paul Mugo na Boniface Wamae walikiuka sheria katika utekelezaji wa majukumu yao na kusababisha makosa yaliochangia kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author