CORD yadai Spika Ethuro alipendelea Jubilee

Mtafaruku umeibuka kuhusu uamuzi wa spika wa seneti Ekwe Ethuro kumruhusu seneta maalum Hoseah Ochwang’i kupiga kura na kusababisha ushindi wa Jubilee kwenye mjadala wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi.  Cord inadai kuwa spika Ethuro alikiuka kanuni za bunge kwa kumnyima Janet Ongera nafasi ya kupiga kura kwa niaba ya Seneta Chris Obure kama alivyoidhinisha seneta huyo kwenye barua iliyoandikwa mwaka 2013. Hata hivyo Ethuro anasema kuwa aliarifiwa na barua aliyopokea muda mfupi kabla ya shughuli ya kupiga kura kuanza na ambayo ilimteua Seneta Ochwangi kufanya jukumu hilo.

Tags:

CORD JUBILEE seneti Ekwee Ethuro sheria ya uchaguzi

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories