Cord yataka makamishna wapya kuchaguliwa


Muungano wa CORD sasa unashinikiza makamishna wa IEBC wanaoondoka wang’atuke mara moja, na wasishiriki kwa njia yoyote katika ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika uchaguzi mkuu ujao. Vinara wa upinzani Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanadai Issack Hassan na kikosi chake wamesalia ofisini na kushawishi utoaji wa zabuni na hivyo basi kujaribu kuvuruga utaratibu na matokeo ya kinyang’anyiro cha mwezi Agosti. Lakini afisa mkuu wa IEBC Ezra Chiloba amesisitiza hakuna sheria yoyote iliyovunjwa, huku makamishna wakisisitiza kusalia ofisini hadi warithi wao wateuliwe.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Treasury allocates Ksh 4.5 B for procurement of vaccines

Avatar
Story By Francis Gachuri
More by this author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *