Duale aandikisha taarifa kuhusu matamshi ya chuki

Kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale anaandikisha taarifa katika makao makuu ya upelelezi wa jinai kuhusu matamshi yanayokisiwa kuwa ya uchochezi wa kikabila. Duale alinukuliwa akiwaelekeza jamii ya Wakamba wasipeleke siasa za Wiper katika kaunti ya Garissa. Viongozi mbalimbali wamemkashifu Duale kuhusiana na matamshi hayo huku mwenyekiti wa tume ya maridhiano Francis Ole Kaparo akitaka uchunguzi kuhusiana na madai hayo kufanyika.

Tags:

WIPER Aden Duale garissa Siasa Kamba Matamshi ya chuki

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories