EACC yanasa gari la kaunti ya Garissa lililokuwa limeibwa


Maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi EACC hii leo wamenasa gari lenye thamani ya shilingi milioni tisa unusu linalosemekana kuibwa kutoka katika serikali ya kaunti ya Garissa.
Kwa mujibu wa maafisa hao gari hilo ambalo limekuwa likizuiliwa katika karakana moja mjini Mombasa lilikuwa miongoni mwa magari 27 yaliyonunuliwa miaka miwili iliyopita ila halikuwasilishwa Garissa kama iliyostahili. Haya yanajiri huku mashirika kadhaa yasiyokuwa ya kiserikali yakipaza sauti zao dhidi ya matumizi mabaya ya pesa za umma kwenye serikali za kaunti.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Patrick Igunza
More by this author