Familia ya Kones yagawanyika kati ya Jubilee na Nasa

Kinyang’anyiro cha ubunge Bomet mashariki kimewavutia wengi kutokana na mama na mwanawe kugombea kiti hicho. Beatrice Kones, aliyekuwa waziri msaidizi wa masuala ya humu nchini na ambaye pia ni mjane wa waziri wa zamani wa barabara Kipkalya Kones, na mwanawe Kevin Kones Kalya, wanagombea kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Jubilee na chama cha mashinani mtawalia. Na kama anavyodadisi mwanahabari wetu Faiza Maganga, ni kivumbi ambacho kinakisiwa na baadhi ya watu kama juhudi za kutafuta kulirejesha jina la familia ya Kones kwenye siasa za Bomet huku wengine wakiashiria malumbano ya kinyumbani katika familia hiyo.

Tags:

Bomet Kipkalya Kones Beatrice Kones

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories