Gavana Obado kusalia korokoroni

Gavana Obado kusalia korokoroni

Gavana wa Migori Okoth Obado, msaidizi wake Micheal Oyamo na karani katika kaunti ya Migori Caspar Obiero, watajua hatma ya iwapo wataachiliwa kwa dhamana siku ya Ijumaa.

Watatu hao wanaokabiliwa na shtaka la mauaji ya Sharon Otieno sasa wameongezewa shtaka la kumuua kijusi aliyekuwa tumboni mwa Sharon wakati wa kuuawa kwake.

Katika kikao kilichofanyika chini ya saa moja mahakamani ya milimani, jaji wa mahakama kuu Jessie Lessit aliwasukuma tena korokoroni Obado, Oyamo na Obiero huku wakisubiri hadi ijumaa, kabla ya kuskizwa kwa ombi lao la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Jacob Ondari ulirekebisha mashtaka na kuongeza mauaji ya mtoto wa miezi saba aliyekuwa tumboni mwa Sharon wakati wa kuuawa kwake.

Watatu hao walikanusha mashtaka mawili ya mauaji na kuomba mahakama kuwaachilia kwa dhamana.

Hata hivyo familia ya Sharon kupitia wakili na mbunge wa Homabay mjini Peter Kaluma, waliwasilisha ombi la kutaka mahakama kufutilia mbali maombi ya watatu hao kuachiliwa kwa dhamana wakisema huenda wakahatarisha maisha yao.

Tags:

obado

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories