George Okode achaguliwa tena kuwa spika wa bunge la Siaya


Bunge la kaunti ya Siaya limeanza rasmi vikao vyake leo ambapo wawakilishi wa wadi wameapishwa na kisha kumchagua spika
Kiapo cha madiwani wapya kimeongozwa na makarani wa bunge hilo. Spika wa bunge lililopita George Okode amefanikiwa kuhifadhi kiti chake baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa kura nyingi. Okode amepata kura 33 huku mpinzani wake wa karibu George Rubik, akipata kura 8. Wengine waliotafuta kiti hicho ni pamoja na Nicholas Abidha na Samuel Muga ambao hawakupata hata kura moja.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Citizen Team
More by this author