Huenda orodha ya mawaziri wapya ikawasilishwa bungeni Jumanne

Huenda baraza la mawaziri litakatangazwa kabla ya krismasi. Inaarifiwa kuwa Rais Uhuru Kenyatta na naibu Rais William Ruto tayari wameshaafikia majina ya watakaoteuliwa kuhudumu katika baraza hilo. Duru zaarifu kuwa majina hayo yatawasilishwa bungeni Jumanne baada ya mkutano wa hapo kesho kati ya Rais Kenyatta, maspika wa bunge na viongozi wa wengi bungeni. Inaarifiwa kuwa bunge litakamilisha uchunguzi wa wateule kufikia tarehe ishirini mwezi huu.

Tags:

President Uhuru Kenyatta Cabinet

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories