Huenda siku ya uchaguzi wa urais ikabadilishwa


Uchaguzi mpya wa urais huenda usiandaliwe tarehe 17 mwezi ujao kama ilivyotangazwa na tume ya uchaguzi nchini-IEBC. Ingawa sababu kadhaa za mabadiliko ya tarehe hiyo zinatolewa na wadau, tarehe mpya ya uchaguzi itaathiri kalenda ya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne inayotarajiwa kung’oa nanga mwezi ujao. Ingawa IEBC haijatangaza tarehe mpya ya uchaguzi wa urais, imewaalika Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa Nasa Raila Odinga au waakilishi wao katika mkutano siku ya Jumatano, kushauriana kuhusu masuala nyeti na maandalizi ya mchuano mpya wa ikulu.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Some MPs plan to shoot down Uhuru\'s proposal on VAT

Story By Francis Gachuri
More by this author