Huenda uchaguzi ukaahirishwa maeneo kadhaa

Tume ya uchaguzi nchini IEBC inapendekeza kuahirisha uchaguzi wa urais katika maeneo yatakayokumbwa na suitafahamu siku ya Alhamisi. Pendekezo hilo lilijadiliwa na kamati maalum iliyobuniwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati katika kikao kilichoandaliwa hapo jana katika ukumbi wa Bomas. IEBC inapendekeza kutumia kipengee 73 cha sheria za uchaguzi, kuahirisha mchuano wa urais haswa katika maeneo yanayomshabikia sana kinara wa nasa raila odinga.

Tags:

IEBC raila odinga Wafula Chebukati Marjan Hussein Marjan

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories