IEBC njia-panda baada ya Odinga kujiondoa na Aukot kujumuishwa


Hali ya mkwamo sasa imeikumba tume ya uchaguzi na shughuli nzima ya maandalizi ya uchaguzi kufuatia msururu wa matukio tangu kinara wa NASA Raila Odinga kubanduka kwenye marudio ya uchaguzi na mahakama kuagiza kuwa Dkt Ekuru Aukot ajumuishwe kwenye uchaguzi huo. IEBC tayari ilikuwa imeshatamatisha shughuli ya kuweka picha na majina ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kwenye mitambo ya KIEMS na ilitizamia kuanza shughuli ya uchapishaji wa karatasi za kupigia kura. Makamishna na mawakili wao wamekuwa kwenye kikao cha siku nzima kutafuta mwelekeo kuhusu suala hili bila nuru kuonekana.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Guns galore

Avatar
Story By Faiza Wanjiru
More by this author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *