IEBC: Wafungwa watasajiliwa kuwa wapigakura

Wafungwa wataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.
Tume ya uchaguzi nchini imesema kuwa itashirikiana na idara ya magereza kuratibu magereza yote nchini kuwa vituo halali vya kupigia kura. Usajili wa wafungwa utafanyika kati ya tarehe 20 na 27 mwezi ujao. Haya yanajiri huku jamii za wafugaji zikipata afueni baada ya IEBC kuweka mikakati ya maafisa wa usajili kuhamisha vifaa vya BVR hadi mahali ambapo wafugaji wamekita kambi. Hata hivyo vifaa vya kuwasajili kilektroniki havitakiuka mipaka ya maeneo bunge yaliyowekwa. Mawakala pia wataruhusiwa kuwaruhusu wanaotaka kubadili maeneo yao ya kupigia kura kufanya hivyo. Mikakati ya usajili wa wakenya wanaoish ughaibuni bado haijaafikiwa huku tume ya iebc ikipanga kukutana na wawakilishi wa kundi hilo wiki ijayo.

Tags:

Usajili wa wapigakura magereza mahabusu

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories