IEBC yatoa zabuni ya ununuzi wa mtambo wa kura

Tume ya uchaguzi nchini-IEBC imeipa kampuni ya Safran Identity and Securities Limited zabuni ya ununuzi wa mtambo wa kuwatambua wapiga kura kielektroniki, siku chacha tu baada ya kukatiza zabuni iliyokuwa imetolewa kwa kampuni ya Gemalto. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema zabuni hiyo imetolewa moja kwa moja kwa kampuni ya Safran, na mtambo huo wa kielektroniki unatarajiwa kuwasilishwa kufikia tarehe 10 mwezi ujao. Hata hivyo, zabuni hiyo ya Ksh 3.8 B huenda ikaibua utata mpya, huku IEBC ikisema walio na tashwishi kuhusu maamuzi yake wako huru kutafuta suluhu mahakamani.

Tags:

IEBC Safran Identity and Securities Limited

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories