IEBC yawasilisha mahakamani stakabadhi zote za uchaguzi wa Okt. 26

Tume ya uchaguzi nchini-IEBC imewasilisha katika mahakama ya upeo, stakabadhi zilizotumika kunakili matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi jana, ambao matokeo yake yamepingwa kwenye kesi zilizowasilishwa na John Harun Mwau, Khelef Khalifa na Njonjo Mue. Stakabadhi hizo ni pamoja na zaidi ya fomu 34A 37,000, fomu 34B 265 na fomu 34C moja. Haya yanajiri huku naibu jaji mkuu Philomena Mwilu akitarajiwa kuteua jopo la majaji watakaosikiza kesi iliyowasilishwa na Okiya Omtata, kushinikiza kufutiliwa mbali kwa zoezi nzima la uchaguzi wa tarehe 26 mwezi jana.

Tags:

IEBC NASA harun mwau PRESIDENTIAL PETITION

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories