Isaac Ruto ajiunga tena na kambi ya Jubilee


Yamkini wasemao husema kwenye ulingo wa siasa, hamna maadui wala marafiki wa kudumu; maslahi tu. Pia, siasa ni mchezo sio tu mchafu bali karata ya hali ya juu, na hili limedhihirika wazi kila wakati mawimbi ya siasa yanapovuma. Inakuwa mtindo wa kutongozana, tukupe nini, na unatuletea nini. Ndiposa baada ya kubandikana majina, kurushiana cheche za matusi , kuanikana peupe, leo wamekumbatiana kwa raha na bashasha. Nazungumzia uhasama wa kisiasa uliokuwepo kati ya Isaac Ruto na William Samoei Ruto. Ni malumbano yaliyochangia Ruto kujiunga na Nasa baada ya kuunda chama chake cha mashinani, lakini leo kama mwana mpotevu amerejea zizini.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Lulu Hassan
More by this author