Jaji Mkuu akanya wanasiasa, vyombo vya habari kujadili kesi ya urais


Jaji mkuu David Maraga amewaonya wanasiasa na wadau mbali mbali dhidi ya kujadili kesi ya uchaguzi wa urais iliyowasilishwa katika mahakama ya juu zaidi nchini-Supereme Court na kinara wa NASA Raila Odinga. Maraga pia amewataka mawakili wa wahusika kwenye kesi hii kuwatahadharisha wateja wao kuhusu athari za kuzungumzia kesi hiyo nje ya mahakama, au jaribio lolote la kuwashurutisha au kuwashawishi majaji kuamua kesi hiyo kwa njia moja au nyingine.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Francis Gachuri
More by this author