Joto la kisiasa lazidi kupanda Nairobi

Jaribio la kuwaunganisha wawaniaji ugavana kaunti ya Nairobi katika muungano wa jubilee hii leo imetibuka baada ya wawaniaji watatu kususia mkutano huo. Seneta wa Nairobi Mike Sonko, mbunge wa Dagoretti Kusini Dennis Waweru na mbunge maalum Johnstone Sakaja hawakuuhudhuria mkutano huo, wakidai kuwa mazungumzo hayo na viongozi wa jubilee ingewafaidi waziri wa maji Eugine Wamalwa na aliyekuwa mbunge wa starehe margaret wanjiru. Mbunge wa Starehe Maina Kamanda Amesema kuwa  hakuna mgombea yeyote  anayependekezwa na muungano na kuwa wote lazima washiriki katika zoezi la mchujo. Stephen Letoo na taarifa hiyo.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories