Jubilee waingia Nairobi
Published on: August 04, 2017 08:22 (EAT)
Rais Uhuru Kenyatta amewahakikishia wenyeji wa Nairobi na taifa kwa jumla usalama wao, huku uchaguzi mkuu ukizidi kubisha hodi. Kenyatta amesema hakuna haja ya Mkenya yeyote kutoroka anapoishi au kufanyia biashara, akihofia ghasia kuzuka na kuagiza vitengo vya usalama kukabiliana na wale wanaochochea uhasama. Jubilee imetetea utendakazi wake miaka minne uongozini, na kuwarai Wakenya kuidhinisha kibwagizo cha Uhuru-Ruto Tano Tena, huku wakiwasuta wapinzani wao kama wasio na dira ya kulielekeza kimaendeleo.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment