Jubilee wakataa maafisa waliotajwa na Chebukati


Mirengo ya Jubilee na Nasa inazidi kuzozana kuhusu maandalizi ya uchaguzi mpya wa urais, kama ilivyoagizwa na mahakama ya juu nchini. Jubilee imepinga mabadiliko ya uongozi katika secretariat ya IEBC, na kudai Marjan Hussein aliyeteuliwa kuongoza shughuli za kinyang’anyiro kipya cha ikulu ni mshirika wa karibu wa Nasa. Kwa upande wake, Nasa inashinikiza kuondolewa kabisa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na wakurugenzi sita wa IEBC, na pia kuhusishwa katika upekuzi wa mitambo ili kufanikisha uchaguzi huru na haki.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Some MPs plan to shoot down Uhuru\'s proposal on VAT

Story By Francis Gachuri
More by this author