Jubilee yadai Raila analenga kugonganisha Wakenya kwa msingi wa ardhi

Suala la ardhi ni mojawapo ya ajenda za kampeini zinazoibua hisia kali na za kihistoria. Na siku 52 kabla ya kipenga cha mchuano wa mwezi Agosti kupulizwa, suala la umiliki wa ardhi limeibuka huku matamshi ya kinara wa NASA Raila Odinga hapo jana katika kaunti ya Kajiado yakiibua mihemko. Viongozi wa Jubilee sasa wanaitaka tume ya maridhiano na utangamano (NCIC) kumchukulia Odinga hatua za kisheria kwa madai ya uchochezi. Hata hivyo, Odinga amekanusha madai hayo, na kudai rais na kikosi chake wanakwepa masuala mazito ya utendakazi wao.

Tags:

raila odinga JUBILEE Kajiado NCIC land injustices ardhi

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories