Kakamega: Mwanaume auawa kufuatia madai ya kutishia wanakijiji maisha

Kakamega: Mwanaume auawa kufuatia madai ya kutishia wanakijiji maisha

Mwanamume mwenye umri wa miaka 33 kutoka kijiji cha Lunyinya eneo bunge la Malava, kaunti ya Kakamega ameuawa na wakaazi kufuatia madai kuwa amekuwa akiwatishia maisha wakaazi wa kijiji hicho.

Mamake Marehemu, Emily Nafula anasema wakaazi wanadai kuwa mtu huyo Elphas Sasaka alikuwa ametoka gerezani ambako alikuwa kwa zaidi ya miezi miwili na aliporudi nyumbani alianza kuwahangaisha wakaazi.

Wanakijiji walifika nyumbani kwa mshukiwa usiku wa manane na kisha kumpiga vibaya. Alifariki alipokuwa anapokea matibabu hospitalini.

Naibu wa Chifu wa kata ndogo ya Lunyinya, George Maina alithibitisha tukio hilo na kuwaonya wakaazi dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories