Kalonzo alikubali kuwa mgombea mwenza kwa masharti
Published on: April 29, 2017 09:23 (EAT)
Kinara wa ODM Raila Odinga atawania urais kwa muhula mmoja tu, na kuwapokeza usukani wenzake katika muungano wa NASA kuanzia mwaka 2022. Kulingana na mkataba uliozinduliwa siku ya Alhamisi, Odinga atajitosa ulingoni katika kinyang’anyiro cha mwaka huu, na iwapo atashinda au asishindwe, chama cha ODM hakitawasilisha mgombea. Suala ibuka ni je, iwapo Odinga atafanikiwa kumlambisha sakafu Rais Uhuru Kenyatta, atakubali kukaa kando baada ya kuchovya buyu la asali ya urais mara moja tu?
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment