Kamama amulikwa
Published on: March 18, 2017 08:30 (EAT)
Mbunge wa Tiaty Asman Kamama ataondolewa kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa kamati ya usalama katika bunge la kitaifa juma lijalo, kutokana na dhana ya kutumia wadhifa wake kuhujumu shughuli za kuwafurusha wahalifu wa wizi wa mifugo kaunti ya Baringo. Licha ya Kamama kusisitiza hana hatia, kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Aden Duale amedokeza kuwa Kamama atahamishiwa katika kamati nyingine, huku ikiarifiwa kuwa mbunge wa Kigumo Jamleck Kamau huenda akaurithi wadhifa huo.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment