Kamati ya bunge yapokea maoni ya umma kuhusu marekebisho ya sheria za uchaguzi
Published on: October 03, 2017 08:19 (EAT)
Kamati ya pamoja ya bunge imeanza kupokea maoni kutoka kwa wananchi na wadau mbali mbali, kuhusu mapendekezo ya kuzifanyia mabadiliko sheria za uchaguzi, kabla ya mchuano mpya wa urais mwezi ujao. Ingawa baadhi ya waliojitokeza leo waliunga mkono mapendekezo hayo, wengine walitilia shaka kiini na nia ya mabadiliko hayo. Aidha, muungano wa NASA umevitaja vikao vya kamati hiyo kama shughuli za Jubilee, zinazokiuka sheria za bunge na katiba.
Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000
Comments
No comments yet.
Leave a Comment