Kamati ya sheria yapendekeza Kinisu atimuliwe

Kamati ya sheria katika bunge la kitaifa imependekeza mwenyekiti wa tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi Phillip Kinisu atimuliwe, kwa kukosa maadili na kuwa na uhusiano wa kibinafsi na kampuni iliyokuwa ikichunguzwa na tume hiyo. Kamati ya Jlac, kwa wingi wa kura, inalitaka bunge kupendekeza Rais Uhuru Kenyatta abuni jopo la kumchunguza kinisu, kwa madai kuwa hakudokeza ana uhusiano na kampuni ya Esaki Limited, iliyokuwa ikichunguzwa kwa kuhusika katika sakata ya huduma kwa vijana(Nys). Francis Gachuri ana taarifa kamili.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories