Kampuni ya magari ya Peugeot kuzindua kiwanda


Kampuni ya magari ya kifaransa ya Peugeot imerejelea shughuli zake humu nchini. Kampuni hiyo imetangaza kufungua kiwanda ambacho kitakuwa kikitengeneza magari elfu moja kila mwaka na kuwaajiri watu mia mbili. Aina tano za magari hayo zitaundwa hususan kwa soko la humu nchini ambapo gari la kwanza linatarajiwa kuwa barabarani mwezi juni mwaka huu. Hafla ya kutia sahihi ushirikiano huo ilifanyika katika ikulu ya Nairobi ikiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: | TALES OF LAMU | Island grappling with an acute shortage of fresh water

Avatar
Story By Citizen Team
More by this author