Karatasi za kura ya urais kuletwa nchini Jumatatu na Jumanne

Karatasi za kupigia kura za urais zinatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatatu na Jumanne wiki ijayo. Hii ni kulingana na kampuni ya Al Ghurair inayochapisha karatasi hizo jijini Dubai. shughuli ya uchapishaji inatarajiwa kukamilika usiku wa leo.
Kwa mujibu Wa tume ya IEBC ndege mbili zitawasilisha karatasi hizo huku ndege nyingine ikisafirisha shehena ya mwisho ya karatasi za michuano ya wadi.
Karatasi za urais zimekuwa zikichapishwa kwa muda wa siku saba zilizopita kufuatia uamuzi wa mahakama ya rufaa wiki iliopita.

Tags:

IEBC Al Ghurair

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories