KCPE: Naibu wa Rais Ruto akagua shughuli ya mitihani

KCPE: Naibu wa Rais Ruto akagua shughuli ya mitihani

Naibu wa Rais William Ruto alikuwa katika shule ya msingi ya Musa Gitau ambapo alisisitiza kuwa hakuna mwanafunzi ambaye atakosa nafasi katika shule ya upili mwaka ujao.

Akisema kuwa serikali itatimiza ahadi iliyotoa kwa wanafunzi. Ruto kisha alisambaza karatasi za mtihani kwa wanafunzi.

Katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang’ ambaye pia alikuwa katika kaunti ndogo ya Kikuyu pia aliwaonya walimu wakuu dhidi ya kuwasajili wanafunzi kutoka shule za kibinafsi kufanya mitihani katika shule za umma.

Kipsang alikuwa ameongoza shughuli ya kufungua kontena za mitihani.

Naye Mkuu wa Sheria Paul Kihara alikuwa katika eneo la Kabete na kusema kuwa licha ya maafisa wakuu serikalini kuwa shuleni kukagua jinsi shughuli ya mitihani inavyoendeshwa, serikali bado inaweka kila juhudi kuangalia jinsi fedha zake zilivyotumiwa katika shule za umma.

Alitoa mfano wa taswira ya shule za umma ambazo ziko katika hali isiyoridhisha licha ya fedha za kutolewa kwa ajili ya shughuli ya ukarabati wa shule.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories