Ken Tarus ateuliwa kaimu afisa mkuu mtendaji wa KPLC

Daktari Ken Tarus ameteuliwa kuwa kaimu afisa mkuu mtendaji na meneja mkurugenzi mpya wa kampuni ya Kenya Power kuanzia leo.

Daktari Tarus atachukua  mahala pa afisa mkuu anayeondoka Ben Chumo ambaye kandarasi yake ya kuhudumu katika kampuni hiyo itakamilika ijumaa wiki hii, baada ya miaka mitatu kileleni mwa kampuni ya Kenya Power. Hadi kuteuliwa kwake, Daktari Ken Tarus alikuwa meneja mkuu katika idara ya fedha katika kampuni ya kenya power. Aidha bodi ya kampuni ya kenya power imesema kuwa imeanza safari ya kumtafuta mrithi wake Ben Chumo, mpango ambao utakamilika hivi karibuni mwaka huu.

Tags:

KENYA POWER Ben Chumo Ken Tarus

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories