

Mwanahabari wa runinga Citizen Jacque Maribe pamoja na Joseph Irungu ambaye ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya Monica Kimani wamefikishwa mahakamani na kukanusha mashtaka ya mauaji ya binti huyo.
Jaji Jessie Lessit aliamuru wawili hao kusalia rumande hadi siku ya Jumatano wakati ambapo ombi la kutaka kuachiliwa kwao kwa dhamana litasikilizwa.
Hata hivyo upande wa mashtaka umetoa sababu kadhaa za kukataa wawili hao kuachiliwa kwa dhamana.
Mawakili wa serikali wamesema kuwa wawili hao hawapasi kuachiliwa kwa kuwa huenda wakatatiza uchunguzi.
Kwa mujibu wa stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani, ukosefu wa makao rasmi ya Joseph Irungu na ushawishi wa Maribe kutokana na kazi yake ya uanahabari huenda zikaingilia uchunguzi.
Na sasa swala nzima la dhamana litapelekwa mbele ya jaji mwingine wa mahakama kuu na kusikizwa siku ya Jumatano.
Also Read:
Wawili hao watasalia rumande hadi siku hiyo ambapo ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana litaangaziwa.
Video Of The Day: | EVENTS 2020 | Raila Odinga’s reflections on 2020 and expectations for 2021 228 views