Kikao cha kwanza cha mahakama ya juu kufanyika Jumamosi


Mahakama ya juu zaidi nchini, hapo kesho itaandaa kikao maalum cha mawakili wa pande zote husika katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais iliyowasilishwa na kinara wa Nasa Raila Odinga. Mada ya kikao cha kesho ni kuweka mikakati ya kusikizwa kwa kesi hiyo, ili kuutumia vyema muda finyu uliopo kubaini iwapo uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta utasalia au wakenya watarejea kwenye debe kwa mchuano mpya wa ikulu.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Francis Gachuri
More by this author