Kikosi cha Jubilee chafanya mkutano kaunti ya Kiambu


Muungano wa Jubilee unataka uchaguzi ufanywe na tume ya uchaguzi nchini kulingana na maagizo ya mahakama licha ya wapinzani kutaka marekebisho kufanyiwa tume hiyo. Wanajubilee wanasema kuwa ni undumakuwili kwa upinzani kufurahia uamuzi uliobatilisha kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na kukataa maagizo yanayohusu marudio kufanywa na IEBC. viongozi hao wanaitaka IEBC kuweka mikakati ya kuwezesha uchaguzi kufanyika haraka iwezekanavyo.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author