Kinara wa Nasa atoa madai mapya dhidi ya serikali

Kinara wa upinzani Raila Odinga amedai wanajeshi wamejumuishwa kwenye njama ya wizi wa kura na chama cha Jubilee. Odinga anayewania urais kwa tiketi ya muungano wa NASA amedai mikutano kadhaa ya kupanga mikakati imeandaliwa na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya nchi kavu na angani, mkuu wa kitengo cha ujasusi (NIS) na mkurugenzi wa kitengo cha upepelezi (CID) ili kubuni mbinu za kumsaidia Rais Uhuru Kenyatta kuhifadhi kiti chake mwezi Agosti. Hata hivyo wizara ya usalama imekanusha madai hayo, huku naibu wa rais William Ruto akimtaja Odinga kama mgombea anayetafuta visingizio kuficha aibu ya kubwagwa kwenye debe.

Tags:

raila odinga NASA

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories