Kivumbi kinatazamiwa kwenye mchujo wa ODM jijini Nairobi


Katika eneo bunge ya Makadara mbunge wa zamani wa eneo hilo Reuben Ndolo na mwenyekiti wa ODM tawi la Nairobi George Aladwa watawania tiketi hiyo ili kumlaza mbunge wa sasa Benson Kangara wa chama cha Jubilee. Katika eneo bunge la Kibra mbunge wa sasa Ken Okoth atatetea kiti chake dhidi ya Eliud Owalo aliyekuwa msaidizi wa kiongozi wa ODM na mgombea urais wa NASA Raila Odinga. Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Simba Arati atapambana na wagombea wawili Elphas Nganyi na Albert Ariku huku kiongozi wa wanafuzi wa chuo kikuu cha Nairobi Babu Owino akikabiliana na mbunge wa sasa George Omondi. Eneo bunge la Lang’ata limevutia wagombea wengi wakiongozwa na Ahmed Ibrahim maarufu papa katika azma ya kunyakua tiketi ya ODM kutoka Joshua Olum ambaye ni mbunge wa sasa. Embakasi kusini itashuhudia kinyanganyiro dhidi ya Irshad Sumra ambaye ni mbunge wa sasa na Kenedy Okeyo.  Abdikadir Mohamed Omar na Abdiaziz Mohamed Hirsi watawania tiketi ya Kamkunji.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: | NEWSNIGHT | Punguza Mizigo, BBI or No Referendum?

Avatar
Story By Citizen Team
More by this author