Korti yasitisha pendekezo la kupunguza mishahara ya wabunge


Mahakama kuu imesitisha kwa muda, utekelezaji wa utaratibu wa kupunguza mishahara na marupurupu ya wabunge ulioasisiwa na tume ya mishahara nchini (SRC). Jaji George Odunga alitoa agizo hilo baada ya tume ya huduma za bunge (PSC) kuwasilisha kesi, na kudai SRC iliwadhulumu wabunge na haikuzingatia gharama yao ya maisha ilipopiga wembe mishahara yao. Kando na kupokea mshahara wa takriban shilingi milioni moja kila mmoja, wabunge sasa wataweza kupokea marupurupu ya usafiri, magari na mikopo ya nyumba.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Francis Gachuri
More by this author