Lusaka na Wangamati wapigwa faini ya Ksh. 1M

Tume ya IEBC imewatoza gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka na mpinzani wake Wycliffe Wangamati wa Ford Kenya faini ya shilingi milioni moja kila mmoja kwa kuchangia katika ghasia za mapema mwezi huu.
Uamuzi huo ambao umetolewa na makamishna watano pia umemtaka mgombeaji huru wa kiti cha ubunge huko Rarieda kulipa faini ya shilingi laki mbili elfu hamsini kwa kutumia rangi za chama cha ODM na picha ya kinara wake Raila Odinga licha ya kuwa alijitenga na chama cha ODM, alipoamua kuwa mgombezi huru.

Tags:

IEBC kenneth lusaka Wycliffe Wangamati

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories