Maadhimisho ya wiki nzima ya walemavu yakamilika


Umati wa watu wakiwemo walemavu wa kusikia walikusanyika hii leo katika uwanja wa Railway Football Club hapa jijini Nairobi ili kuadhimisha siku ya walemavu wa kusikia ulimwenguni.
Leo ikiwa ni mwisho wa maadhimisho ya wiki moja kuhusu walemavu wa kusikia ulimwenguni, walikusanyika kufanya matembezi ya Amani kutoka jumba la KICC hadi uwanja wa Railway football club.
Kampeni hizi za watu walio na ulemavu wa kusikia unalenga kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujua lugha ya ishara na kuwatambua watu wanaoishi na ulemavu katika katiba ya taifa hili.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Citizen Team
More by this author