Maafisa wa IEBC wazuiwa kutoa mafunzo huko Bondo


Huenda tume ya uchaguzi ikafutilia mbali uchaguzi wa terehe 26 katika baadhi ya maeneo ambapo usalama wa maafisa wa uchaguzi unatiliwa shaka. Haya ni baada ya maafisa kususia mafunzo na baadhi kutimuliwa na makundi ya watu katika maeneo ya Nyanza na magharibi mwa nchi. Naibu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha anasema kuwa tume hiyo itatathmini vitisho dhidi ya maafisa wake kabla ya kutoa mwelekeo. Haya ni huku mahakama ya upeo ikisema kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hana mamlaka yoyote ya kubadilisha matokeo ya uchaguzi.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: | BULLDOZERS FOR SANITIZERS | Families remain in the cold after evictions from Kariobangi sewage estate

Avatar
Story By Faiza Wanjiru
More by this author