Maandalizi ya mitihani ya KCPE, KCSE

Maandalizi ya mitihani ya KCPE, KCSE

Wizara ya Elimu kwa ushirikiano na baraza la mitihani nchini KNEC imeweka mikakati kabambe kuhakikisha mitihani ya kitaifa mwaka huu inaandaliwa kwa njia sawa.

Hii leo waziri wa elimu Amina Mohamed amekutana na waakilishi kutoka KNEC, wazazi na wamiliki wa shule za kibinafsi kupanga mikakati hiyo, huku akiwaonya wazazi dhidi ya kuwatembelea wanafunzi shuleni muhula huu wa tatu.

Aidha, wanafunzi watakaopatikana na simu ya rununu shuleni hawatasazwa.

Hata hivyo juhudi za wizara ya elimu na KNEC zimepata changamoto kutoka kwa baadhi ya watu wenye njama ya kuiba mitihani na wale wenye mipango ya kusambaza karatasi ghushi kwa wazazi na wanafunzi.

Mwenyekiti wa baraza la mitihani Profesa George Magoha amesisitiza kuwa mitihani iko salama na wanaweka kila juhudi kuhakikisha mitihani inafanywa katika mazingira inayopasa.

Aidha waziri Amina alisema kuwa serikali inaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mitihani inawafikia wanafunzi wote katika maeneo tofauti nchini.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories