Magaidi waangamiza watu 4 huko Hindi, Lamu


Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab wamewaangamiza watu 4 katika eneo la hindi kaunti ya Lamu. Mashambulizi hayo yamefanyika katika vijiji viwili tofauti, kisa cha kwanza kilifanyika katika kijiji cha Bobo mwendo wa saa kumi na mbili na nusu siku ya Jumanne na kingine kufanyika mwendo wa saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha silini-mashambani.
Wanamgambo hao walikuwa na bunduki aina ya AK 47, na walizunguka vijiji hivyo wakiamuru watu kutoka katika nyumba zao kabla ya kutekeleza mauaji. Kulingana na kamishna wa kaunti ya lamu, gilbert kitiyo hali hii ni ya kutamausha kwani wanamgambo hao walikuwa wakitaja majina ya wahanga wao kabla ya kuwachinja. Haya yanajiri huku operesheni ya kuwasaka magaidi hao ikiendelea.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Former sports CS Hassan Wario convicted over Rio games scam

Avatar
Story By Citizen Team
More by this author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *