Mahakama yaamua kambi ya Dadaab isifungwe

Uamuzi wa kenya kufunga kambi ya Dadaab umepata pigo baada ya mahakama kuamuwa kwamba uamuzi huo ulikuwa unakiuka haki za binadamu. Vile vile serikali imetakiwa kuidhinisha tena idara ya wakimbizi na kuhakikisha kwamba shughuli zinaendelea kama kawaida katika kambi hiyo. Uamuzi huo uliotolewa na Jaji John Mativo hata hivyo umepata pingamizi huku msemaji wa serikali Eric Kiraithe akidai kwamba watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwani kulingana nao ni kwamba hatua hiyo iliafikiwa kwa sababu ya usalama wa taifa.

Tags:

Dadaab John Mutivo

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories